Amini Mitume Wake

Sura ya Biblia ya kila siku

Majadiliano

Wakati wa Kusoma: 2 minutes Sikiliza Mtandaoni Right arrow icon

1 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
10 Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
11 Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
12 Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
13 Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
14 Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
15 Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
16 Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
17 Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
18 Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
19 Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
20 Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
21 Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
22 Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
23 Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
24 Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
25 Kila chenye mwili akipa chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 
26 Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

See Previous Reading See Next Reading

JIUNGE NA MJADALA