Amini Mitume Wake

Sura ya Biblia ya kila siku

Majadiliano

Wakati wa Kusoma: 2 minutes Sikiliza Mtandaoni Right arrow icon

1 Tena neno la Bwana likanijia, kusema, 
Mwanadamu, kaza uso wako juu ya mlima Seiri, ukatabiri juu yake, 
uuambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee mlima Seiri, nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, nami nitakufanya kuwa ukiwa na ajabu. 
Miji yako nitaiharibu, nawe utakuwa ukiwa; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. 
Kwa kuwa umekuwa na uadui usiokoma, nawe umewatoa wana wa Israeli wapigwe kwa nguvu za upanga, wakati wa msiba wao, wakati wa mwisho wa uovu. 
Basi, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, nitakuweka tayari kwa damu, na damu itakufuatia; ikiwa hukuchukia damu, basi damu itakufuatia. 
Hivyo ndivyo nitakavyoufanya mlima Seiri kuwa ajabu na ukiwa; nami nitakatilia mbali nao mtu apitaye, na mtu arejeaye. 
Nami nitaijaza milima yake watu wake waliouawa; katika milima yako, na katika mabonde yako, na katika mifereji yako ya maji yote, wataanguka wao watakaouawa kwa upanga. 
Nitakufanya kuwa ukiwa wa daima, na miji yako haitakaliwa na watu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. 
10 Kwa sababu umesema, Mataifa haya mawili na nchi hizi mbili zitakuwa zangu, nasi tutazimiliki, ijapokuwa Bwana alikuwako huko. 
11 Basi, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, nitatenda kwa kadiri ya hasira yako, na kwa kadiri ya wivu wako, ulioudhihirisha kwa kuwachukia; nami nitajidhihirisha kwao, nitakapokuhukumu wewe. 
12 Nawe utajua ya kuwa mimi, Bwana, nimeyasikia matukano yako yote, uliyoyanena juu ya milima ya Israeli, ukisema, Wamefanyika ukiwa, wametiwa katika mikono yetu tuwale. 
13 Nanyi mmejitukuza juu yangu kwa vinywa vyenu, na kuyaongeza maneno juu yangu; nimesikia mimi. 
14 Bwana MUNGU asema hivi; Dunia yote itakapofurahi, nitakufanya kuwa ukiwa. 
15 Kama vile ulivyofurahi juu ya urithi wa nyumba ya Israeli, kwa sababu ilikuwa ukiwa, ndivyo nitakavyokutenda wewe; utakuwa ukiwa, Ee mlima Seiri, na Edomu yote, naam, yote pia; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.

See Previous Reading See Next Reading

JIUNGE NA MJADALA