Hosea 12
Soma sura Jiunge na Majadiliano
Ufafanuzi
Mimi ni mtoto wa kati. Sikupata marupurupu ya kuwa Kifungua mimba na wala sikuwa mziwanda au kitinda mimba nidekwe. Ninahisi kama nilipaswa kupigania haki yangu kwa kila kitu. Hiyo inaweza kuonekana ilifanya kazi kwa viwango kadhaa kama mtoto lakini pia ilikuwa na bei yake - nilijifunza kuwaona wengine kama wapinzani. Nilipokuwa Mkristo, niligundua kuna njia nyingine ya kuishi: katika ushirika na kwa kushirikiana na Mungu.
Hosea 12: 3 , ikimtaja Yakobo, inasoma, "Alimpiga mwereka ndugu yake tumboni, na akiwa mtu mzima alipigana na Mungu." Biblia zingine (version) hufanya iwe kama Yakobo na Bwana walikuwa wanapigana wakiwa karibu, lakini tunajua kwamba Yakobo alipigana dhidi ya Bwana. Haikuwa mpaka Yakobo alipojua alikuwa ameshindwa nguvu ndipo akabadilika kutoka kupigana na Bwana na kushikamana na Bwana. Swali langu ni, Kwanini inapaswa kufikia hatua hiyo? Kwa nini mwitikio wetu wa kwanza kwa Mungu ni adui badala ya ushirikiano? Mtazamo huu mbaya ni sehemu yetu ya asili ya mwanadamu mwenye dhambi. Mungu anaweka wazi kuwa anataka kutuokoa na kutubariki. Yesu anasema, "Njooni kwangu ... nami nitawapumzisha." Mathayo 11:28.
Karen D. Lifshay
Katibu wa Mawasiliano ya Kanisa, Hermiston, Oregon USA