Amini Mitume Wake

Sura ya Biblia ya kila siku

Majadiliano

Wakati wa Kusoma: 2 minutes Sikiliza Mtandaoni Right arrow icon

1 Ee Bwana, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu. 
Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni; Na nyumba zetu kuwa mali ya makafiri. 
Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; Mama zetu wamekuwa kama wajane. 
Tumekunywa maji yetu kwa fedha; Kuni zetu twauziwa. 
Watufuatiao wa juu ya shingo zetu; Tumechoka tusipate raha yo yote. 
Tumewapa hao Wamisri mkono; Na Waashuri nao, ili tushibe chakula. 
Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao. 
Watumwa wanatutawala; Hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao. 
Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu; Kwa sababu ya upanga wa nyikani. 
10 Ngozi yetu ni nyeusi kama tanuu; Kwa sababu ya hari ya njaa ituteketezayo. 
11 Huwatia jeuri wanawake katika Sayuni; Na mabikira katika miji ya Yuda. 
12 Wakuu hutungikwa kwa mikono yao; Nyuso za wazee hazipewi heshima. 
13 Vijana huyachukua mawe ya kusagia; Na watoto hujikwaa chini ya kuni. 
14 Wazee wameacha kwenda langoni; Na vijana kwenda ngomani. 
15 Furaha ya mioyo yetu imekoma; Machezo yetu yamegeuka maombolezo. 
16 Taji ya kichwa chetu imeanguka; Ole wetu! Kwa kuwa tumetenda dhambi. 
17 Kwa sababu hiyo mioyo yetu imezimia; Kwa ajili ya hayo macho yetu hayaoni vema. 
18 Kwa ajili ya mlima Sayuni ulio ukiwa, Mbweha hutembea juu yake. 
19 Wewe, Bwana, unadumu milele; Kiti chako cha enzi ni tangu kizazi hata kizazi. 
20 Mbona watusahau sikuzote; Na kutuacha muda huu mwingi? 
21 Ee Bwana, utugeuze kwako, nasi tutageuka; Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale. 
22 Isipokuwa wewe umetukataa kabisa; Nawe una hasira nyingi sana juu yetu.

See Previous Reading See Next Reading

JIUNGE NA MJADALA