Mika 7
Soma sura Jiunge na Majadiliano
Ufafanuzi
Je! Kusikiliza taarifa ya habari kunakuongezea kukata tamaa? Tunasikia visa kutoka duniani kote za utakasaji wa kabila kitamaduni (culture cleansing) inayouhusiana na mauaji , vita, njaa, na misiba. Kwa hakika Mika alihisi kukata tamaa, lakini anafarijika kwamba kutakuwa na malipo mwishowe na yuko tayari kuingojea hiyo siku.
Kitabu cha Mika kinafunga kama kilivyoanza, kwa kutia moyo kwamba hukumu inakuja na mambo yatafanywa sawa. Kwa hivyo hukumu ni habari njema!
Mtume Paulo anazungumzia juu ya hukumu na injili pamoja: "Hii itafanyika siku ambayo Mungu atahukumu siri za watu kupitia Yesu Kristo, kama injili yangu inavyotangaza" (Warumi 2:16, NIV). Hukumu ni sehemu ya habari njema ya injili.
Katika Ufunuo, malaika analeta habari njema ya hukumu inayokuja: "Mcheni Mungu na kumtukuza, kwa kuwa wakati wa hukumu Yake umewadia ." (Ufunuo 14: 7).
Hukumu hiyo ni habari njema kwa sababu uamuzi ulitolewa pale msalabani. Tunakaribia kiti cha enzi cha neema ya Mungu kwa ujasiri kwa sababu tumefunikwa na vazi la haki ya Kristo. Yesu ndiye kuhani wetu mkuu, jaji, mwanasheria, na mtetezi Na hatupaswi kuogopa.
Gordon Bietz
Rais (mstaafu)
Chuo Kikuu cha , Southern Adventist College, Tennessee