Zaburi 120
Soma sura Jiunge na Majadiliano
Ufafanuzi
Zaburi zinazofuata (120-134) zinajulikana kama Zaburi za mpando au nyimbo za ‘kwenda juu’. Wana wa Israeli walizoea kuziimba Zaburi hizi walipokuwa katika safari ya kurudi kutoka hija Yerusalemu katika zile siku kuu tatu ambazo ambazo waliagizwa kuadhimisha kila mwaka. (angalia Kumbu Kumbu la Torati 16:16) Hebu jaribu kupiga picha mawazoni mwako na ujione ukisafiri kwenye vilima vilivyozunguka Yerusalemu ukiwemo katika msafara wa waumini wengine waliochoka, na mnajiunga pamoja katika kuimba, mkitazamia kuliona hekalu la Mungu, mahali ambapo Mungu alisema lijengwe ‘ili akae na watu wake’. Nyimbo hizi ziliiimbwa na makuhani pia wakiingia hekaluni wakati wa ibada.
Hata nasi leo tu wasafiri kuelekea mbinguni nyumbani kwetu kule ambako tutaishi milele kama vile ahadi thabithi tulizopewa na Mungu zinavyotukumbusha.; kadiri tunavyosafiri, ni vyema kutambua kwamba sisi ni wahitaji, tunamhitaji YEYE Mungu. Tujikumbushe kwamba dunia hii si kwetu kama Mwandishi wa Zaburi anavyosema kwenye Zaburi 120:5
Safari yetu yenye uchovu inaburudishwa na kufanywa rahisi endapo tunashirikiana na wale ambao Mungu ametusaidia wawe wenzi au marafiki zetu katika safari. Je kuna mtu ambaye Mungu amekusaidia atembee nawe?. Je kuna yoyote ambaye anakusaidia kwa kuimba nyimbo za kukutia moyo? Mungu asifiwe Mungu ashukuriwe kwa rehema zake na kwa wenzi aliotupa tutembee nao pamoja kwenye safari yetu ya kwenda mbinguni na kuifanya iwe rahisi kwa kiasi fulani.
Cindy Nash
Mke, Mama, Nesi
Collegedale, Tennessee, Marekani